“Jeshi la Sudan Kusini limefanya jinai kubwa”
Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa zaidi ya watu milioni mbili na laki mbili, raia wa Sudan Kusini wamelazimika kuyakimbia makazi yao ambapo laki sita kati yao wamekimbilia katika nchi jirani za Ethiopia, Kenya na Uganda. Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imeongeza kuwa, karibu asilimia 70 ya jamii ya watu milioni 12 wa Sudan wanakabiliwa na matatizo ya usalama wa chakula.
Sudan Kusini ilitumbukia katika machafuko tangu mwezi Disemba mwaka 2013 baada ya Rais Salva Kiir wa nchi hiyo kumtuhumu makamu wake wa zamani kwa kupanga njama ya kutaka kumpindua, machafuko ambayo yamepelekea maelfu ya watu kuuawa.
(chanzo tehran radio idhaa ya iswahil)
Post A Comment
Hakuna maoni :