
Chama cha wananchi CUF nchini tanzania ambacho ni miongoni mwa vyama
vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA kimekanusha kuwa
kimesusia vikao vya umoja huo ambavyo vimeendelea kikisema kwanza
kinataka kurejea katika katiba yao ili wafanye maamuzi kwa mujibu wa
katiba ya chama hicho. Haya yanajiri baada ya baadhi ya vyombo vya
habari na mitandao ya kijamii kuripoti kuwa chama hicho kimejiengua
kutoka katika umoja huo kwa madai kuwa chama hicho hakijapewa nafasi ya
kuteuwa mgombea ikizingatiwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho Profesa
Ibrahim Lipumba
ana sifa za kuwakilisha umoja huo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 25.
(DW idhaa ya kiswahili)
Post A Comment
Hakuna maoni :