technology

Binti wa miaka 10 na ajuza wajilipua Nigeria

Binti wa miaka 10 na ajuza wajilipua NigeriaBinti mdogo aliyekuwa na umri wa miaka 10 na ajuza mmoja siku ya Ijumaa walitekeleza mashambulio ya kigaidi kwa kujilipua huko kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuuwa makumi ya watu. Kanali Sani Usman msemaji wa jeshi la nchi hiyo amesema kuwa mlipuko huo wa kigaidi uliotokea katika soko la mji wa Gombe ulioko kaskazini  mashariki mwa Nigeria ulitekelezwa na binti aliyekuwa na umri wa miaka 10 na ajuza mmoja ambao wote ni wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram. Awali maafisa wa nchi hiyo walitangaza kuwa milipuko miwili ya kigaidi ilikuwa imetokea katika eneo hilo na kusababisha maafa ya watu 50 na kujeruhi wengine 70. Tokea kuingia madarakani Rais Muhammad Buhari wa Nigeria na kuahidi kupambana vilivyo na Boko Haram, kundi hilo limezidisha operesheni zake za kigaidi nchini humo ambapo mamia ya watu wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa.
(CHANZO tehran radio )
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :