CNN yafichua namna US inavyowapa mafunzo Daesh
Televisheni ya Marekani ya CNN
imefichua habari inayosema kuwa, Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo
imewapa mafunzo magaidi wa Daesh. Televisheni hiyo ya Marekani
imesambaza mkanda wa video kupitia Intaneti ambapo ndani ya mkanda huo
anaonekana Kanali Gulmurod Khalimov, mkuu wa zamani wa jeshi la polisi
la Tajikistan ambaye hivi sasa amejiunga na kundi la kigaidi la Daesh
akisema kuwa, yeye binafsi ameshiriki mara tatu katika mafunzo ya
kijeshi ndani ya ardhi ya Marekani na moja ya mafunzo hayo ameyapata
kwenye jimbo la Louisiana la Marekani. Hata Wizara ya Mambo ya Nje ya
Marekani imekiri jambo hilo. Msemaji mmoja wa Wizara ya Mambo ya Nje ya
Marekani ameiambia televisheni ya CNN kwamba Kanali Khalimov alipata
mafunzo ya kijeshi katika vipindi vitano tofauti nchini Marekani na
Tajikistan baina ya mwaka 2003 hadi 2014. Amesema, mafunzo hayo
yalitolewa na kusimamiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kwa kile
alichodai ni kupambana na ugaidi. Licha ya viongozi wa Marekani kukiri
mara kwa mara kuwa ndio waliolianzisha na kulipa mafunzo kundi la
kigaidi la Daesh lakini hivi sasa wameunda muungano wa kulipiga vita
kundi hilo. Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, huo ni mchezo wa kisiasa
tu wa Marekani, na kwamba Washington na waitifaki wake hawana nia ya
kweli ya kupambana na kundi hilo la kigaidi
Post A Comment
Hakuna maoni :