technology

Maiti za wakimbizi 100 zapatikana pwani ya Libya


Maiti za wakimbizi 100 zapatikana pwani ya LibyaShirika la Hilali Nyekundu la Libya limetangaza kuwa maiti za karibu wakimbizi mia moja zimepatikana katika pwani ya nchi hiyo.
Msemaji wa Shirika la Hilali Nyekundu la Libya, Mohamed al-Masrati, amesema kuwa maiti za watu 95 zimepatikana katika pwani ya Libya katika siku kadhaa zilizopita. Al Masrati ameongeza kuwa 85 kati ya maiti hizo zimepatikana katika pwani ya mji mkuu wa Libya, Tripoli na nyingine 10 zimekutwa katika pwani ya mji Sabartha.
Shirika la Hilali Nyekundu la Libya linasema wengi kati ya wahanga hao walikuwa wakimbizi kutoka nchi za Kiafrika waliokuwa wakijaribi kuingia Ulaya kupitia Libya.
Katika miezi ya hivi karibuni maelfu ya wakimbizi, wengi wao wakiwa ni kutoka nchi za Afrika na Mashariki ya Kati, wamekimbia nchi zao zilizokumbwa na machafuko na vita vya ndani wakitaka kuingia katika nchi za Ulaya. Maelfu miongoni mwao wamefariki dunia kwa kuzama baharini.

chanzo-tehran radio
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :