technology

Lubuva: Wasimamizi wa uchaguzi fuateni sheria

Lubuva: Wasimamizi wa uchaguzi fuateni sheriaMwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC), Jaji Damian Lubuva amewataka wasimamizi wa uchaguzi na makamanda wa polisi wa mikoa yote nchini, kufuata sheria ya uchaguzi na kutenda haki; na haki hiyo ionekane ikitendeka siku ya uchaguzi mkuu. Aliyasema hayo jana jiji Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi na makamanda wa polisi wa mikoa yote nchini na kanda maalumu wapatao 800. Alisema ni vyema kujifunza kutokana na makosa yaliyotokea kwenye chaguzi zilizopita ili katika uchaguzi huu mambo hayo yasijirudie.
Alisema uchaguzi wa mwaka huu unapaswa kufanyika kwa amani na uhuru na kuhakikisha kuwa hawaruhusu vitendo vya uvunjifu wa amani au vile vinavyoonesha hatari ya kuvunjika kwa amani. Amevita vyama vya siasa na mawakala wao kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na NEC, za kuwataka wananchi wakishapiga kura waondoke vituoni kwani jukumu la ulinzi wa kura ni la tume hiyo na mawakala wao.
chanzo-tehran radio
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :