7:20am: Usalama umeimarishwa katika
kituo kikuu cha kujumlisha matokeo katika ukumbi wa Julius Nyerere.
Tume inatarajiwa kutoa matokeo ya kwanza saa tatu. Image caption
Masanduku ya kupigia kura
7:15 am: Mjini Mwanza, kaskazini
magharibi mwa Tanzania, masanduku ya kura yanaendelea kukusanywa katika
afisi kuu kabla ya kuanza kwa shughuli ya kuhesabu kura. Image caption
Uchaguzi tanzania
7.00 am: Maafisa wanaanza kuingia
mmoja mmoja kituo cha kupigia kura Kimara Stop Over, Dar es Salaam
ambako wapiga kura wanatarajiwa kupiga kura zao za urais na ubunge baada
ya uchaguzi kutatizika jana. Wapiga kura walifikia kituoni tena mapema
sana leo. Image caption
Raia wa kwanza
6.00 am: Kituo cha Kimara Stop Over
jijini Dar es Salaam ambako uchaguzi unafaa kufanyika leo baada ya
kutatizika jana, maafisa wa kusimamia uchaguzi bado hawajafika kituoni. Tume
ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania imesema itaanza kutoa matokeo rasmi ya
uchaguzi wa urais leo saa tatu katika jumba la mikutano la Julius
Nyerere, Dar es Salaam. Hata hivyo kuna maeneo ambayo uchaguzi
haukufanyika Jumapil
NI MWANDISHI WA TOP NEWS BLOG, AMESHAFANYA KAZI YA UANDISHI NA UTANGAZAJI KATIKA KITUO CHA RADIO-PANGANI FM RADIO,LAKINI KWA SASA ANAENDELEA NA ELIMU YA JOURNALISM KATIKA NGAZI YA DIPLOMA-MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGORO-TANZANIA
Post A Comment
Hakuna maoni :