Korti yakataa kuzuia kura ya maamuzi Rwanda

Mahakama ya Juu nchini Rwanda imetupilia mbali kesi ya kupinga mpango wa kufanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo kumruhusu Rais Paul Kagame kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Kesi hiyo ilikuwa imewasilishwa na chama cha upinzani cha Green Party.
"Kesi hii…haina msingi wowote na imetupwa,” shirika la habari la AFP limemnukuu Jaji Mkuu Sam Rugege akisema.
Wabunge walikubaliana mwezi Julai kufanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo na kuandaa kura ya maamuzi kuhusu suala hilo.
"Kwanyima watu uhuru wa kuamua jinsi watatawaliwa si demokrasia, ni kinyume cha demokrasia,” jaji huyo amesema.
Rais Kagame ameongoza kwa mihula miwili ya miaka saba baada ya kushinda uchaguzi 2003 na 2010.
chanzo-bbcswahili.com
chanzo-bbcswahili.com
Labels
kimataifa
Post A Comment
Hakuna maoni :