Cameroon yaua wapiganaji 100 wa Boko Haram

Afisa huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa oparesheni kali imefanyika dhidi ya ngome za Boko Haram usiku wa jana na leo Alfajiri ambapo takriban magaidi 100 wameuawa. Duru za kiintelijensia zinasema kuwa, jeshi la Cameroon lilipokea taarifa kuhusu ngome za Boko Haram katika eneo la mpakani na kwa mantiki hiyo likapanga oparesheni ya kushtukizia.
Kundi hilo la kigaidi lilishambulia eneo la Kangeleri kaskazini mwa Cameroon mwanzoni mwa wiki na kusababisha vifo vya watu 9.
Post A Comment
Hakuna maoni :