technology

Boko Haram yaua watu 40 Chad

Image copyrightReuters
Image captionBoko Haram yaua watu 40 Chad
Maafisa wa hospitalini wanasema zaidi ya watu 40 wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa kufuatia msururu wa milipuko nchini Chad.
Image copyrightAFP
Image captionMajeshi ya Chad, ambao wanaisaidia serikali ya Nigeria kupambana na wapiganaji hao
Mashambulio hayo yamelenga soko na kambi ya wakimbizi iliyoko eneo la Baga Sola ufuoni mwa ziwa Chad.
Image copyrightReuters
Image captionMashambulio hayo yamelenga soko na kambi ya wakimbizi iliyoko eneo la Baga Sola
Kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Boko Haram,limetuhumiwa kwa kutekeleza mashambulizi hayo.
Mashambulizi hayo ya mabomu yalitokea katika mji ulioko Chad karibu na mpaka na Nigeria.
Image captionKambi ya wakimbizi iliyoko eneo la Baga Sola ufuoni mwa ziwa Chad ililengwa
Raia wengi wa Nigerian walitorokea eneo hilo kujaribu kujinusuru kutoka kwa mashambulio ya wanamgambo hao.
Lakini kundi hilo Boko Haramu limekuwa likiendeleza mashambulio hadi nchi jirani kama Chad, ambao wanaisaidia serikali ya Nigeria kupambana na wapiganaji hao.
Benin, Cameroon, Chad, Niger na Nigeria ziliafikiana kuchangia kikosi cha muungano chenye askari jeshi 8,700 japo kuna madai huenda ukosefu wa ufadhili ndio uliochangia kikosi hicho kutoanza kazi yake.
chanzo-bbcswahili.com
Post A Comment
  • Blogger Comment using Blogger
  • Facebook Comment using Facebook
  • Disqus Comment using Disqus

Hakuna maoni :