Wananchi wa Yemen wamefanya maandamano makubwa mjini Sana'a kulalamikia
mashambulizi ya kinyama ya Saudia dhidi ya nchi yao. Maandamano hayo
makubwa yamefanyika baada ya kiongozi wa harakati ya Ansarullah, Sayyid
Abdul Malik al Houthi kutoa mwito kwa wananchi hao kujitokeza kwa wingi
kwenye maandamano kulaani jinai za Saudi Arabia dhidi ya nchi yao.

Katika hotuba yake aliyoitoa kwa njia ya televisheni, al Houthi amesema
kuwa, utawala wa ukoo wa Aal Saud wa Saudi Arabia unafanya jinai
zilezile zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi
madhlumu wa Palestina. Sayyid Abdul Malik al Houthi ametoa hotuba hiyo
kuadhimisha mwaka wa kwanza tangu yalipofanyika mapinduzi ya wananchi
nchini Yemen na kusema kuwa, adui Mzayuni asingelithubutu kukivunjia
heshima kibla cha kwanza cha Waislamu yaani Masjidul Aqsa, kama si uadui
wa Saudia dhidi ya wananchi wa Yemen. Amesema ukoo wa Aal Saud
unashirikiana na Israel katika mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuuzamisha
umma wa Kiislamu kwenye dimbwi la matatizo na fitna za kitaifa, ili
Waislamu wasifikirie kabisa suala la kukomboa kibla chao cha kwanza huko
Palestina kutoka katika makucha ya utawala ghasibu wa Kizayuni. Amesema
Saudi Arabia inashirikiana na Israel kulitumbukia eneo hili kwenye vita
na kwamba anayefaidika pekee kwenye machafuko na vita hivyo ni utawala
wa Kizayuni wa Israel.
chanzo-http://kiswahili.irib.ir/habari
Post A Comment
Hakuna maoni :