
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu amesema uzembe uliofanywa na
serikali ya Saudi Arabia ndio uliosababisha tukio la maafa yaliyotokea
katika mji mtukufu wa Makka. Katika ujumbe maalumu aliotoa jana Ali
Larijani, mbali na kutoa salamu za rambirambi kwa Waislamu kufuatia
tukio la kusikitisha la Makka alitoa mkono wa pole pia kwa familia za
wafanyaziara waliopoteza maisha na kueleza kwamba serikali ya Saudia
ilipaswa ichukue hatua za lazima kuhakikisha usalama wa mahujaji, lakini
uzembe iliofanya umesababisha kutokea tukio hilo. Spika wa bunge la
Iran ameeleza katika ujumbe wake huo kwamba maafa hayo ya kusikitisha
yamezitonesha na kuziungulisha nyoyo za umma wa Kiislamu na kuichanganya
Hijja ya Kiibrahim na simanzi na majonzi na kwamba kuna udharura wa
kufanyika uchunguzi unaohitajika juu ya tukio hilo. Watu wasiopungua 107
walifariki dunia na wengine wasiopungua 238 walijeruhiwa siku ya Ijumaa
baada ya winchi kuangukia msikiti mtukufu wa Makka. Wafanyaziara watano
kutoka Iran ni miongoni mwa waliofariki dunia katika tukio hilo…
chanzo-tehran radio
Post A Comment
Hakuna maoni :