
Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM) imesema
inaunga mkono miradi ya nyuklia ya Iran ikiwemo haki ya Tehran ya
kurutubisha madini ya urani. Taarifa iliyotolewa jana kwenye kikao cha
mwezi huu cha Bodi ya Magavana ya wakala wa IAEA na Reza Najafi
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika wakala huo
imetilia mkazo misimamo mikuu ya harakati ya NAM, ikiwemo haki muhimu na
isiyoweza kutenganishwa ya nchi zote duniani ya kustafidi na nishati ya
nyuklia kwa malengo ya amani na kueleza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran ina haki ya kutumia teknolijia ya nyuklia kwa malengo ya amani.
Taarifa iliyotolewa Reza Najafi katika kikao cha Bodi ya Magavana ya
IAEA imeongeza kuwa: Harakati ya NAM imepokea vizuri makubaliano
yaliyofikiwa kati ya Iran na kundi la 5+1 na inaamini kuwa makubaliano
hayo yatasaidia kutatua kwa amani kadhia ya nyuklia ya Iran.
(Tehran radio)
Post A Comment
Hakuna maoni :