Rais Kikwete asema nchi za Afrika hazitaweza kuendelea bila kuboresha miundombinu.

Rais Jakaya Kikwete amesema nchi za Afrika hazitaweza kuzungumzia
mipango ya maendeleo bila ya kuboresha miundombinu na mifumo
itakayowezesha upatikanaji na matumizi sahihi ya takwimu kwa ajili ya
maendeleo.
Akifungua mkutano wa kwanza wa kimataifa wa takwimu huria kufanyika
Afrika uliohudhuriwa na nchi zaidi 30, rais Kikwete amesema takwimu ni
nyenzo muhimu ya maendeleo na hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana
bila ya matumizi ya takwimu sahihi kwa vile zinazewezesha kutambua
changamoto za kijamii na kiuchumi na kusisitiza moja ya changamoto za
nchi za Afrika ni upatikanaji wa takwimu sahihi.
Awali waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhe. Mathias Chikawe amesema
katika ulimwengu wa digitali takwimu huria imekuwa moja na nyezo muhimu
katika kuimarisha uwazi na uwajibikaji na kupeleka huduma kwa jamii
ikiwa ni pamoja na kuendeleza ubunifu ambapo amesema moja na malengo ya
mkutano huo ni kubadilishana uzoefu na wadau kutoka nchi mbalimbali
wakiwemo asasi za kirai, serikali na sekta binafsi.
Aidha akizungumza na waandishi wa habari, katibu mkuu kiongozi
balozi Ombeni Sefue amesema mfumo wa takwimu huria unawezesha
upatikanaji wa takwimu za serikali kwa uwazi ambapo Tanzania imeanza na
wizara ya afya, maji na elimu kwa kuwa zinagusa jamii moja kwa moja na
kusisitiza mpitia mfumo huo wananchi wanaweza kuihoji serikali na
kuiwajibisha.
(itv.co.tz)
Post A Comment
Hakuna maoni :