KUTUMIKISHWA KWA WATOTO KATIKA SHUHULI ZA UVUVI TANGA BADO CHANGAMOTO...........
Tatizo la kuwatumikisha
watoto katika shughuli ya uvuvi katika
kijji cha kipumbwi wilayani pangani bado linaendelea hali inayo pelekea watoto
hao kukosa elimu na kuhatarisha maisha yao.
Akiongea na PANGANI FM
MMOJA wa wananchi katika mkutano ulioitishwa na SHIRIKA LISILO
LA KISERIKALA LA SEA SENSE linalo toa
elimu juu ya uhifadhi wa rasili mali
bahari na utunzaji wa mazingira ,amesema hali hiyo ipo na inasababishwa na
baadhi ya familia kuwa na kipato kidogo
hivyo wazazi kuwa achia watoto wao kwenda baharini.
Hata hivyo katibu wa
BMU katika kijiji cha KIPUMBI ndugu MUSA OMARI MASUDI amekiri
kuwepo kwa tatizo hilo na kwa
upande wake yeye amesema tatizo la watoto kwenda baharini lina sababishwa na manahoza kuwatumia watoto hao kwa kuwalipa
ujira mdogo.
Na kwa upande wake
mwenyekiti wa kitongoji ndugu HASANI MUHAMMED amesema yeye anapata wasiwasi juu
ya suala hili na amewataka manahodha kuacha tabia ya kuwatumikisha watoto
katika uvuvi.
Tatizo la kutumikishwa
kwa watoto katika kijiji cha kipumbwi katika uvuvi linaendelea kuchukua sura
mpya kutokana na kijiji cha kipumbwi
kutokua na sheria yoyote ya kudhibiti suala hili la watoto wa shule za
msingi na sekondari kutoka katika maeneo ya SAKURA,MTONGA,MAKARAWE na SANGE kwa
ajili ya uvuvi.
Labels
KITAIFA
Post A Comment
Hakuna maoni :