IS kwenye headline tena yateka kambi ya wanahewa wa Syria
Ripoti kutoka nchini Syria zinasema
kuwa kambi moja ya jeshi la wanahewa kaskazini mwa nchi imetekwa na
wanamgambo wa Islamic state.
Kambi hiyo ilikuwa imezungukwa kwa kipindi cha miaka miwili.
Runinga ya taifa nchini Syria inasema kuwa wanajeshi waliondoka katika kambi ya Abu Duhur iliyoko kwenye mkoa wa Idlib. Image copyrightReuters
Wanajeshi hao waliondoka baada ya mashambulizo ya kila mara kutoka kwa kundi la Nusra Front
Wanajeshi hao waliondoka baada ya mashambulizo ya
kila mara kutoka kwa kundi la Nusra Front lenye uhusiano na kundi la
kigaidi la Al Qaeda.
Kambi hiyo ilikuwa kituo cha mwisho kilichokuwa kikidhibitiwa na serikali katika mkoa wa Idlib.
NI MWANDISHI WA TOP NEWS BLOG, AMESHAFANYA KAZI YA UANDISHI NA UTANGAZAJI KATIKA KITUO CHA RADIO-PANGANI FM RADIO,LAKINI KWA SASA ANAENDELEA NA ELIMU YA JOURNALISM KATIKA NGAZI YA DIPLOMA-MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGORO-TANZANIA
Post A Comment
Hakuna maoni :