
Kongamano la kimataifa la kukabiliana na makundi yenye kufurutu ada
limeanza nchini Mauritania. Kongamano hilo lililoanza jana Jumatano
linafanyika mjini Nouakchott, mji mkuu wa nchi hiyo. Wasomi, watafiti na
mahatibu kutoka nchini za Ulaya, eneo la Sahel mwa Afrika, Marekani na
baadhi ya nchi za Kiafrika, wanahudhuria kongamano hilo la siku mbili na
lililofunguliwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Yahya Ould Hademine.
Akihutubia kongamano hilo, Sheikh Abdallah bin Bayyah mmoja wa wasomi
wakubwa wa Mauritania alizitaka nchi za dunia kutenga bajeti
itakayodhamini mahitaji katika sekta ya utamaduni kwa lengo la kuwazuia
vijana na wasichana kujiunga na makundi yenye kufurutu ada na ambayo
yanatekeleza jinai dhidi ya binaadamu kwa jina la Uislamu. Aidha Sheikh
Bin Bayyah amesema kuwa hii leo ulimwengu unahitajia sana kuliko wakati
mwingine wowote, kuandaliwa mipango ya kiutamaduni na kiusalama sanjari
na kufuatwa mwenendo wa mazungumzo ya usawa baina ya pande hasimu badala
ya kufuata mwenendo wa mapigano na mauaji. Aidha washiriki wa kongamano
hilo litakalomaliza shughuli zake hii leo, wamelaani jinai za makundi
ya kigaidi na kitakfiri hususan Daesh, Boko Haram na Jab’hatu Nusra.
(chanzo tehran radio idhaa ya kiswahili.com)
Post A Comment
Hakuna maoni :