
Kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh nchini Iraq, limebomoa msikiti
mmoja kusini mwa mkoa wa Nainawa, sanjari na kuondoa nakshi za
kihistoria katika makanisa mawili katikati ya mji wa Mosul. Kwa mujibu
wa kanali ya Sumaria News, kundi la Daesh limefanya uharibifu huo
Jumamosi ya jana baada ya kuulipua kwa bomu Msikiti wa Abubakar katika
viunga vya eneo la al-Shura, kusini mwa mkoa wa Nainawa. Matakfiri hao
wasioelewa mafundisho ya dini ya Kiislamu, mbali na kukiri kutekeleza
jinai hiyo, wamesema kuwa wameubomoa msikiti huo kutokana na kile
walichokitaja kuwa ni kuwepo kaburu ndani yake. Wanachama wa kundi hilo
maarufu kwa kutenda jinai pia wameondoa maandishi ya kihistoria katika
makanisa mawili ya Bikira Maria na al-Kaldan, katikati mwa mji wa Mosul
mkoani Nainawa nchini Iraq. Kabla ya hapo wanachama wa Daesh walifanya
mauaji dhidi ya wapiganaji 20 wa kundi hilo mjini Mosul, kwa makosa
tofauti ukiwemo usaliti. Si vibaya kukumbusha kuwa, mji wa Mosul umekuwa
ukidhibitiwa na wanachama wa kundi hilo la kitakfiri tangu tarehe 10
Juni mwaka 2014, suala ambalo limepelekea mji huo kukumbwa na hali mbaya
ya kibinadamu kutokana na wanachama wa kundi hilo kutekeleza sheria
kali za kufurutu ada katika mji huo.
(tehran radio)
Post A Comment
Hakuna maoni :