
Huku viongozi wa Kenya na makundi ya kiraia yakiendelea kumuonya Rais wa
Marekani, Barack Obama, dhidi ya kuishinikiza nchi yao ikubali ndoa za
watu wa jinsia moja wakati atakapokuwa Nairobi mwishoni mwa mwezi huu,
ikulu ya White House mjini Washington imesisitiza kuwa, kiongozi huyo
ataligusia suala hilo wakati wa ziara yake hiyo. Msemaji wa Rais Obama,
Josh Earnest, amesema kiongozi huyo hatosita kuelezea mtazamo wake
kuhusu suala la ushoga. Naibu Rais wa Kenya, William Ruto, Spika wa
bunge la Kitaifa, Justin Muturi na mwenzake wa Seneti, Ekwe Ethuro ni
miongoni mwa viongozi waandamizi wa Kenya ambao wamemuonya Obama dhidi
ya kuishinikiza nchi yao kuwakubali mashoga. Makumi ya wabunge na
mashirika mengi ya kiraia pia yanamtaka Obama kuheshimu utamaduni wa
Wakenya na Waafrika na kujiepusha kuzungumzia suala hilo
atakapoitembelea Kenya Julai 25. Spika wa bunge la kitaifa amesema bunge
litachukua hatua iwapo Obama atadharau mila na utamaduni wa Wakenya
chanzo (tehran radio idhaa ya kiswahili)
Post A Comment
Hakuna maoni :