MWINGEREZA AFELI MAJARIBIO AZAM FC,NAFASI YAKE KUCHUKULIWA NA MKENYA
Mambo yameshaharibika kwani lile dili la
kiungo Ryan Burge kutaka kuwek a rekodi ya kuwa Muingereza wa pili kucheza Ligi
Kuu Bara limeshindikana na muda wowote ataondoka nchini kurudi kwao.
Kally Ongala, ndiye raia wa kwanza wa
Uingereza, kucheza Ligi Kuu Bara alipozichezea Yanga na Azam, kabla ya kuachana
na soka na sasa ni kocha.
![]() |
WANGA (MBELE) WAKATI AKIWA EL MERREIKH AKIPAMBANA NA MIGI WAKATI AKIICHEZEA |
Taarifa zinaeleza baada ya ujio wa Allan Wanga,
Azam FC imeona ni vizuri kumchukua Mkenya huyo na kuachana na Mwingereza huyo.
Burge alisema: “Muda wowote nitaondoka kurejea nyumbani kwa sababu kuna timu imetokea kunihitaji, siwezi kukutajia ni timu gani mpaka nitakapofika huko na kufanya nao mazungumzo.”
chanzo salehjembe.blospot.com
Post A Comment
Hakuna maoni :