WAASI SUDANI KUSIN WADAI KUTUNGUA NDEGE YA UGANDA
Waasi wa Sudan Kusini wamedai kuidungua helikopta ya kijeshi ya jeshi la
Uganda na kuua marubani wawili pamoja na wanajeshi wote waliokuwemo
ndani ya ndege hiyo.
Waasi wanadai jeshi la Uganda linapambana kuusaidia upande wa serikali ya Sudan Kusini.
Hata hivyo taarifa hiyo iliyotolewa na msemaji wa waasi hao Dickson Gatluack haikutowa maelezo juu ya idadi kamili ya waliokuwemo ndani ya ndege hiyo. Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini Phillip Aguer amekiri kwamba mji wa Kodok unadhibitiwa na waasi kwa sasa ila amekanusha taarifa za kuangushwa kwa helikopta ya jeshi la Uganda.

Post A Comment
Hakuna maoni :