
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (Unesco)
limeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kuanzisha uchunguzi
kuhusu kubomolewa na makundi ya wanamgambo makaburi ya kale huko
kaskazini mwa Mali. Irina Bokova Mkurugenzi Mkuu wa Unesco amesema kuwa
kuharibiwa urithi wa kiutamaduni kunachukuliwa kuwa ni jinai ya kivita
kwa mujibu wa makubaliano ya The Hague ya Umoja wa Mataifa ya mwaka
1954. Mwaka 2012 wanamgambo wanaobeba silaha waliuteka mji wa Timbukutu
yapata umbali wa kilomita 1000 kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Mali
Bamako na kubomoa makaburi ya masharifu wa Kiislamu ya karne ya 15 na
16. Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Unesco amesema kuwa miezi miwili
iliyopita alikutana na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa mahakama ya ICC na
kwamba anaamini kuwa mahakama hiyo inafanya jitihada za kufanya
uchunguzi kuhusu kuharibiwa urithi huo wa kitamaduni huko kaskazini mwa
Mali na kesi hiyo kuanza kusikiliza mahakamani. Tawi la kiutamaduni la
Umoja wa Mataifa limeanza kuujenga upya mji wa kihostoria wa Timbuktu
unaojulikana kwa jina la mji wa watakatifu 333 kwa msaada wa serikali ya
Mali na taasisi nyingine za kimataifa, baada ya wanamgambo wenye silaha
kundoka mjini humo kufuatia oparesheni za kijeshi za mwaka 2013.
tehran radio idhaa ya kiswahili.com
Post A Comment
Hakuna maoni :