Mashambulizi mapya yauwa zaidi ya 30 Nigeria
Mashambulizi mapya ya watu wenye silaha wasiofahamika katika
jimbo la Zamfara kaskazini magharibi mwa Nigeria yameua watu 32, hiyo
ikiwa ni katika muendelezo wa mashambulizi ya kigaidi yanayoikumba nchi
hiyo ya magharibi mwa Afrika. Mwenyekiti wa serikali za mitaa katika
jimbo la Zamfara Muhammad Gusami amethibitisha kutokea mashambulizi hayo
makubwa huko Gasua makao makuu ya jimbo la Zamfara.
Afisa huyo amesema kuwa, watu waliokuwa na silaha walivishambulia vijiji vya Kokeya na Chigama baada ya kujipenyeza vijijini hapo kwa kutumia pikipiki, na kisha wakawauwa wanavijiji wawili na kuchoma moto nyumba kadhaa na kuiba baadhi ya mifugo, wengi wakiwa ng’ombe.
Muhammad Gusami ameongeza kuwa, wavamizi hao baadaye walirudi tena katika eneo hilo na kuingia katika kijiji jirani cha Chigama na kuua watu zaidi ya 30.
chanzo tehran radioidhaa ya kiswahili

Post A Comment
Hakuna maoni :