Waziri wa masuala ya Nje wa Marekani
John Kerry amekashifu matokeo ya uchaguzi ya Burundi yaliyotolewa hapo
jana ambapo rais Pierre Nkurunziza alitangazwa kusajili ushindi mkubwa.
Kerry
ametaja uchaguzi huo kuwa ukiukaji mkubwa wa katiba na kejeli kwa mfumo
wa haki huku akimlaumu rais Pierre Nkurunziza kwa ghasia zilizotokea
nchini humo wiki chache kabla ya kufanyika uchaguzi. Rais Nkurunziza alitangazwa mshindi na asilimia 70 ya kura
Katika taarifa kwa vyombo vya
habari saa chache zilizopita, waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani
amesema kuwa amesikitishwa kwa namna rais Nkurunziza ameiponda katiba ya
nchi na kupuuza mkataba waliosaini mjini Arusha miaka kumi na tano
iliyopita.
Amesema kuwa rais huyo ametumia mbinu ghushi kung'ang'ania madarakani katika uchaguzi ambao sio huru wala wa haki.
Kerry anasisitiza kuwa mazungumzo ya amani yafanyike
Kerry amesisitiza kuwa ni
lazima pande zote husika nchini humo zirudi katika majadiliano ya dhati
na kuhusisha pia mashirika ya kijamii.
Amesema kuwa hii ndio njia
ya pekee ya kurejesha imani sio tu ya raia wa Burundi bali jamii ya
kimataifa pia, na kuzuia ghasia zaidi nchini humo zilizosababisha watu
kuikimbia nchi.
Hapo jana tume huru ya uchaguzi nchini Burundi
ilitangaza kuwa rais Nkurunziza amepata asilimia karibu sabini ya kura
zilizopigwa katika uchaguzi huo uliofanyika siku ya Jumanne wiki hii. Kerry amesisitiza kuwa ni lazima pande zote husika nchini humo zirudi katika majadiliano
Kura katika majimbo zinatarajiwa kutangazwa katika kipindi cha wiki moja ijayo.
Viongozi
wakuu wa upande wa upinzani nchini Burundi walisusia uchaguzi
huo,lakini majina yao yalisalia katika karatasi za kupigia kura.
Kiongozi wa upinzani Agathon Rwasa alimaliza katika nafasi ya pili akizoa asilimia kumi na tisa ya kura zilizopigwa.
NI MWANDISHI WA TOP NEWS BLOG, AMESHAFANYA KAZI YA UANDISHI NA UTANGAZAJI KATIKA KITUO CHA RADIO-PANGANI FM RADIO,LAKINI KWA SASA ANAENDELEA NA ELIMU YA JOURNALISM KATIKA NGAZI YA DIPLOMA-MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGORO-TANZANIA
Post A Comment
Hakuna maoni :