CECAFA:Gor Mahia yainyamazisha Yanga

Shakava alifunga bao la kusawazisha baada ya kufunga kichwa kizuri kutoka kwa mkwaju wa adhabu uliopigwa na Karim Nizigiyimana baada ya Godfrey Walusimbi kuangushwa upande wa kushoto kunako dakika ya 18 kabla ya Olunga kuimarisha mambo na kuiweka Gor kifua mbele dakika moja baada ya kipindi cha mapumziko.
Nahodha wa timu ya Yanga Nadur alikosa penalti katika kipindi cha pili baada ya Shakava wa Gor Mahia kuunawa mpira katika eneo la hatari huku kipa wa Gor Mahia akiudaka mkwaju wake kwa urahisi.
Katika mechi nyingine ya ufunguzi, KMKM ya Zanzibar waliwafunga Telecom ya Djibouti 1-0 katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume.
APR ya Rwanda pia iliwafunga Al-Shandy ya Sudan 1-0 katika mechi iliyoanza kabla ya ile ya Yanga vs Gor Mahia katika uwanja wa Taifa.
(chanzo bbcswahili.com)
Post A Comment
Hakuna maoni :