Saudia inashambulia kwa silaha zilizopigwa marukufu

Shirika hilo limetoa ripoti yake leo
Jumapili baada ya maafisa wake kutembelea mkoa wa Sa’ada wa kaskazini
mwa Yemen na kusema kuwa, Saudia imekuwa ikitumia mabomu ya vishada
kuwalenga raia na maeneo ya makazi ya watu wa kawaida.
Shirika hilo lenye makao yake nchini
Marekani limesema kuwa, Saudia imetumia aina tatu tofauti za mabomu
yaliyopigwa marufuku ya vishada dhidi ya raia wa Yemen.
Shirika hilo limesambaza pia picha
zinazoonesha mabaki ya mabomu ya vishada yaliyotumiwa na Saudia kwenye
maeneo mbalimbali ya Yemen kama vile al Nushoor na al Maqash, mkoani
Sa’ada, kaskazini mwa Yemen.
Post A Comment
Hakuna maoni :